1 Imbeni nyote siva za Bwana,
Na njoni kwake, Ee dunia.
Shangelieni nyote pamoja,
Atumkiwe kwa furaha.
2 Bwana ni Mungu, jueni nyote;
Alituumba, si wenyewe,
Na sisi sote tu watu wake,
Tu kondoo wake sisi sote.
3 Nyuani mwake na malangoni,
Ingieni na usukuru.
Mshukuruni, shangilieni,
Na jina lake lisifuni.
4 Kwa kuwa wema ni wake Mungu,
Hata milele ni karimu.
Uaminifu wa Bwana wetu,
Vizazi vyote utadumu.
Source: Nyimbo Za Imani Yetu #8