Text: | Mjini kwake Babangu |
Author: | Mch. Sila Msangi |
1 Mjini kwake Babangu
Ndipo pa raha
Tutafika juu kwake
Tukae naye.
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Lini tutafika kwake
Tuungane na malaika
Mjini kwake, mjini kwake.
2 Pale kwake Babngu
Ndipo pazuri
Siku ile kuu mno
Ya kupaona.
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Mji ung'arao mno
Ni makao ya maliaka
Mjini kwake, mjini kwake.
3 Nikipanda mlimani
Na kuyaona
Yote ya utukufu
Aliyofanya.
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Yote yanisimulia
Ufahari wake Baba
Mjini kwake, mjini kwake.
4 Njoo mwenzangu tazama
Yote ya Mungu
Yote ameyafanya
Kwa ajili yetu
Kuna raha Kuna raha,
Kuna raha Kuna raha,
Tuinue macho yetu
Tumtazame mwumba wetu
Mjini kwake, mjini kwake.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Mjini kwake Babngu |
Title: | Mjini kwake Babangu |
Author: | Mch. Sila Msangi |
Refrain First Line: | Kuna raha Kuna raha |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kujuta na kutegemea: Kutegemea |